Siku moja baada ya kuteuliwa kwa
wakuu wa Wilaya Madiwani wa Halimashauri ya Wilaya ya Tarime wamemkataa Mkuu wa
Wilaya ya Tarime John Henjewele na kumuomba Rais Jakaya Kikwete aweze kumuondoa
katika Wilaya hiyo na kumpangia Wilaya nyingine ya kufanyia kazi baada ya
kushindwa kudhititi usalama wa Raia na mali zao na kufanya ukaidi kila
anaposhauriwa.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari
mara baada ya kuhailishwa kwa kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani
kilichokuwa kifanyike katika ukumbi wa mikutano wa Halimashauri hiyo,Madiwani
hao walidai kuwa DC Henjewele akiwa kama Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama ameshindwa kudhibiti matukio ya mauajia ambapo hivi karibuni katika
mgodi wa Nyamongo na Tarime Mjini lakini Mekaa kimya.
Kiongozi wa upinzani katika Baraza
la madiwani wa Halimashauri hiyo Ndesi Charles wa kata ya Turwa (CHADEMA)
alisema wameamua kwa kauli moja kutokufanya kikao cha Baraza la Madiwa kutokana
na DC huyo kuigeuza Halimashauri ya Tarime kama Taasisi yake na kusema kuwa
hawataendesha vikao vya Baraza hilo mpaka hapo mkuu wa Mkoa atakapokuja na
kuondoka na DC huyo.
Ndesi amesema kuwa wameshangazwa na
uteuzi uliofanyika jana wa ma DC na Henjewele kuendelea kubakishwa katika
Halimashauri hiyo licha ya taarifa ya kulalamikiwa na Wananchi pamoja na
Madiwani kwa kushindwa kuzingatia utawala bora na kuendelea kukumbatiwa.
"Madiwani wote tumeamua kwa
pamoja kugomea kufanya kikao hicho ambacho kilikuwa na ajenda ya kupitia
taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) lakini tumeshindwa kufanya
na hatutafanya mpaka hapo DC Henjewele atakapoondolewa katika Wilaya ya
Tarime,"alisema Ndesi.
Alisema DC Henjewele kwa sasa
anafanya biashara zake na amewekeza katika mgodi wa Nyamongo na kushindwa
kufatilia kelo za Wananchi na kufikia hatua ya kuzuia wawekezaji waliopo
kuatika mgodi huo wa ABG kukataa kulipia karo za wanafunzi kama ilivyo katika
makaubaliano na mgodi huo.
Diwani wa kata ya Nyamaraga Antony
Manga (CCM) alisema suala la DC huyo lilishaongelewa katika vikao vya chama
lakini ameshindwa kuwa msikivu katika masuala ya msingi anayolalamikiwa na
Wananchi pamoja na Madiwani hivyo nao wameamua kwa pamoja kumkataa na sio
chaguo sahihi kwa Tarime katika dhana nzima ya kuhalakisha maendeleo.
Amesema kumekuwa na kero mbalimbali
zinazomuhusu ikiwemo kutokusikiliza kuondolewa kwa kizuizi cha Nkende kata ya
Sirari ambacho kimekuwa kikwazo kikubwa kwa wafanyabiashara kufanya shughuli
zao za kimaendeleo kutokana na kuwepo kwa kizuizi hicho na kudai kuwa kizuizi
cha Kirumi kinatosha.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Halimashauri ya Wilaya ya Tarime na Diwani wa kata ya Sirari Amos Sagara
amesema kutokufanyika kwa kikao hicho cha kawaida cha Baraza la Madiwani ni
baada ya kutokea kwa marumbano ya madiwani wote kabvla ya kikao wakitaka
kutokufanyika kwa kikao hicho mpaka hapo atakapokuja mkuu wa Mkoa ili aweze
kuondoka na DC huyo kutokana na madai yao mbalimbali juu yake.
Alisema baada ya maluymbano hayo
kuzidi aliamua kuhitisha kikao cha ndani na Madiwani wote na kupitisha azimio
moja la kutokufanyika kwa kikao hicho mpaka hapo watakapowasiliana na Mkuu wa
Mkoa ili kushiriki katika kikao cha pamoja na Madiwani hao ili kuweza kufikia
muafaka wa yale yanayozungumzwa.
Akiongea kwa njia ya simu, Henjewele
alisema yale yote yanayolalamikiwa na Madiwani hao si ya kweli na kama
wanataarifa za kimaandishi wanapaswa waziwasilishe na si kuongea mambo ambayo
hayana ukweli na kudai kuwa huenda wanazo sababu zao nyingine.
Alisema kuwa hali ya kiusalama
katika Wilaya ya Tarime ni nzuri na hayo wanayo yaongea na kufikia hatua ya
kugomea kikao juu yangu si ya kweli na kuendele kusisistiza kama wanao ushahidi
juu ya hayo yote waweze kuyatolea taarifa kwa njia zinazo stahili.
SIASA TU HAPO AKUNA LOLOTE
ReplyDelete