TANZANITE Foundation ambayo ni kampuni
tanzu ya TanzaniteOne ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara imechangia
maendeleo ya jamii kwenye kijiji cha Naisinyai kwa kujenga shule
mbili,zahanati,visima vya maji na kituo cha jamii.
Akizungumza wakati akigawa vifaa vya
shule na michezo kwa wanafunzi wa shule ya msingi New Vision ya mji mdogo wa
Mirerani,Mkurugenzi wa Tanzanite Foundation Hayley Henning alisema lengo lao ni
kusaidia jamii na siyo kupata faida.
Henning aliongoza na wageni kutoka
nchini Marekani wakiwemo waandishi wa habari Robert Weldan Weldo wa Gia na
Steve Bennett wa Gems Tv alisema wapo kwa ajili ya kuimarisha na kudumisha
imani na uadilifu wa Tanzanite.
No comments:
Post a Comment