MWANAMUZIKI nyota wa Tanzania wa Bongo flava, Naseeb Abdul
‘Diamond Platnumz” juzi usiku aliweza kuuteka umati wa wageni maalum uliofurika
kwenye ukumbi wa jumba la shindano la Big Brothe stargame, na afrika kwa
ujumla kwa kupiga shoo kali na ya aina yake ,nchini Afrika Kusini.
Katika shoo hiyo ambayo pia ilishuhudiwa na mamilioni ya
watazamaji, ulimwenguni kote kupitia ving’amuzi vya Dstv, Diamond aliweza
kudhihirisha uwezo wake huo kwa kuangusha bonge la shoo ikiwemo kwa wimbo
wake wa ‘Mawazo’ ambao uliwachanganya watu mbalimbali na kuamka vitini
mwao na kupanda jukwaani na kucheza nae.
Diamond kama kawaida yake, aliweza kuvalia vilivyo, alikonga
nyoyo za mashabiki hao kwa staili yake ya uchezaji ikiwemo ya kuigiza kama anaanguka pamoja na ile ya miondoko ya msanii wa
Orijino komed, Joti, hadi anamaliza shoo hiyo mashabiki hao walikua na hamu ya
kumuona na kusikia nyimbo zake.
Awamu ya pili, Mshereheshaji mkuu wa shindano hilo,
Osakioduwa maalufu, IK, aliweza kumwita tena jukwaani Diamond ilikuzungumza
machache, Diamond bila hiyana aliwashukuru mashabiki kwa sapoti waliompa na
kuwapongeza wote.
“Nimefarijika sana,nawapendeni wote Big brother, funs, na
wote” alisema Diamond na baadae IK, alimuomba apige wimbo wa mwisho wa kufungia
shoo hiyo na kuporomosha kibao cha ‘Moyo wangu’ ambacho nacho kiliwachanganya
zaidi mashabiki huku kivutio lkikubwa kikiwa juu ya uchezaji wake huo wa
Kijoti.
Katika shoo, hiyo, mshiriki wa Zambia, Mampi aliweza kutolewa
kufuatia kupata kura chache zilizopigwa baada ya kuingia kwenye hatari yeye na
wenzake wawili,Maneta na Lady May.
big up Diamond platnum coz kibao cha mawazo kinamfariji sana Agness n Glory japo Renie hampendi kiivyo Diamond platnum...
ReplyDeletehongera sana Diamond Platnim kibao cha mawazo huwa kna waliwaza sana Agness n Glory however Renie hampend kiivyo
ReplyDelete