
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Dk. Terezya Huvisa
ameiasa jamii ya watanzania kujenga tabia ya kupanda na kutunza miti
ili kufaidika na biashara ya hewa ukaa.
Dk.
Huvisa ameyasema hayo mwishoni mwa wiki katika Wilaya ya Mufindi
mkoani Iringa alipofanya ziara ya kikazi kukagua miradi inayotekelezwa
na Kampuni ya Green Resources katika vijiji vya Idete na Uchindile
Amezitaja
faida za misitu kuwa ni uuzaji wa hewa ukaa ambayo kwa kiasi kikubwa
hupatia wananchi fedha kwa ajili ya huduma muhimu za maendeleo ikiwa ni
pamoja na ujenzi wa shule, zahanati, na kutoa ajira kwa jamii
inayozunguka.
Dk.
Huvisa amewasihi wananchi wa Mufindi kutumia utaalamu wa wawekezaji
hao katika kuandaa mashamba yao ya miti na kudumisha uhusiano mzuri
baina yao na wawekezaji. “msiuze ardhi yenu yote kwa wawekezaji bali
tumieni fursa hiyo kuandaa mashamba yenu kitaalamu ili muweze kunufaika
pia” Alisisitiza Dk. Huvisa.
Akitoa taarifa kwa Waziri, Meneja wa Mradi wa Green Resource
Bw Sangito Sumari, amesema kiasi cha Shilingi bilioni moja zimetolewa
na kampuni hiyo kusaidia miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi
wa Shule ya Awali, Barabara, na miradi ya Maji katika vijiji vya Idete,
Mapanda, Uchindile, Makungu na Chogo.
Kuhusu
biashara ya hewa ukaa katika mwaka 2010, “Kampuni imetoa asilimia kumi
kwa ya mauzo ya hewa hiyo kwa vijiji vya wilaya ya Mufindi na
Kilombero ambapo kijiji cha Chogo kilipata sh. Milion 10 , Mapanda milioni 30, Uchindile Milioni 75 na Kitete 10 milioni,” alisisitiza Bw. Sumari.
Kampuni ya Green Resources
inafanya kazi zake katika nchi ya Tanzania, Uganda na Msumbiji na
inajishughulisha na upandaji wa miti, uvunaji wa hewa ukaa na mradi wa
kuzalisha na kusambaza umeme unaandaliwa.
No comments:
Post a Comment