Msanii wa filamu nchini
Elizabeth Michael a.k.a Lulu akiwa Mahakamani mapena leo wakati alipofika
kusikiliza mashtaka yake yanayomkabili kuhusiana na tuhuma za mauaji ya msanii
mwenzake,Marehemu Steven Kanumba Lulu akiwa mahakamani hapo.Lulu akiwasili
Mahakamani hapo.
Mahakama Kuu kanda ya Dar es
salaam imepanga kutatoa uamuzi juu ya umri wa msanii wa filamu nchini Elizabeth
Michael maarufu kwa jina la Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii
mwenzake Steven Kanumba Aprili 7 mwaka huu.
Jaji Fauz Twaib leo
alisikiliza mapingamizi ya mawakili wa serikali kuhusiana na maombi ya mawakili
wanaomtetea Lulu waliyowasilisha mahakamani hapo kuiomba korti hiyo aidha
ichunguze umri wa Lulu anayedai ana miaka 17 au iamuru mahakama ya kisutu
kuchunguza.
Baada ya kuwasilishwa maombi
hayo leo ilikuwa ni siku ya kusikilizwa maombi mahakamani ambapo wakili
Shadrack Kimaro wa Serikali alipinga vikali maombi hayo kuwepo mahakamani hapo
akidai kuwa hayakustahili kuwepo na badala yake yatupwe.
Alidai walichofanya ni
kinyume cha sheria ilipaswa wakate rufaa kwasababu maombi yalishafika mahakama
ya kisutu inakosikilizwa kesi hiyo na kutolewa maamuzi hivyo haikuwa sahihi
kufungua maombi mapya wakati sio maombi mapya.
Aliwashauri mawakili wa Lulu
aidha kukata rufaa maamuzi ya Kisutu au kuomba maamuzi yale kufanyiwa mapitio.
Hata hivyo alidai kifungu cha sheria kilichotumika kuwasilisha maombi hayo sio
sahihi ilipaswa kitumike kifungu ambacho kitaipa mamlaka korti hiyo kusikiliza
maombi.
Mawakili wa Lulu, Furgence
Masawe, Peter Kibatala na Kennedy Fungamtama hawakukubaliana na hayo,ambapo
Fungamtama aliiomba mahakama kupokea maombi yao
na kutolea uamuzi kwasababu ndiko maombi yao
yanakotakiwa kupelekwa.
Aliusoma upya uamuzi
uliotolewa Kisutu na kudai kuwa haukuwa uamuzi bali maelekezo ya mahakama na
wao wamefata maamuzi hayo yaliyowataka kuwasilisha maombi yoyote Mahakama Kuu
kwasababu mahakama ile haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji.
Baada ya kusikiliza mabishano
hayo ya kisheria mahakama hiyo imepanga kutoa maamuzi Juni 16 mwaka huu
No comments:
Post a Comment